Hamasishwa na taarifa za Taswira ya Mtaa
Zanzibar
Tazama kikundi cha wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa, “World Travel in 360 (WT360)” wakizungumza kuhusu Project Zanzibar, mpango wa pamoja na serikali ya Tanzania wa kuweka Zanzibar kwenye ramani. Federico Debetto, Nickolay Omelchenko na Chris du Plessis walisafiri Tanzania ili kukagua jinsi ya kuweka funguvisiwa kwenye ramani, kuelimisha wakazi kuhusu picha za Taswira ya Mtaa na kujenga muundo thabiti kwa jamii ili iendeleze mpango huu kivyake.
Myama
Gundua Myama kupitia video hii inayoonyesha kazi nzuri ya mpigapicha Nyi Lynn Seck na wenzake kutoka 3XVIVR Productions. 3XVIVR walitumia muda na juhudi nyingi katika mpango wao maalum, wakilenga kuweka Myama mtandaoni kupitia Taswira ya Mtaa na kuhifadhi turathi za kitamaduni katika picha za digrii 360.
Zimbabwe
Mtazame Tawanda Kanhema akisimulia taarifa yake kuhusu kuweka Zimbabwe kwenye ramani akitumia Taswira ya Mtaa. Tawanda alirudi nchi yake ya Zimbabwe akiwa na lengo la kuweka picha za Taswira ya Mtaa za mji wa Harare (mji mkuu) na Victoria Falls (kivutio maarufu kwa watalii wa kimataifa) kwenye Ramani za Google. Hivi karibuni amepanua mradi wake ili kujumuisha pia maeneo mengine makuu katika Zimbabwe.
Kenya
Kutana na baadhi ya Wajuzi wa Mitaa na wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa wanaoweka Kenya kwenye ramani. Ari yao ya kuusaidia ulimwengu ujue kuhusu uzuri wa ajabu wa nchi ya Kenya iliwapelekea wachague Taswira ya Mtaa kama zana bora zaidi ya kutimiza lengo hili.
Armenia
Sikiliza Joe Hacobian, mmoja wa waanzilishi wa shirika lisilo la faida la Armenia360. Joe alizungumza kwenye Mkutano wa Taswira ya Mtaa 2019 jijini London kuhusu safari ya timu yake ya kuweka nchi ya mababu zao kwenye ramani. Hii ni taarifa kuhusu jinsi mtu yeyote anavyoweza kuweka maeneo anayothamini kwenye ramani kwa kutumia Taswira ya Mtaa.
Bamuda
Pata maelezo kuhusu jinsi Mamlaka ya Utalii ya Bamuda, shirika linalotangaza maeneo ya utalii, limeipa kazi Miles Partnership shirika la kuaminika la Taswira ya Mtaa ili kukusanya picha za Taswira ya Mtaa. Miles Partnership wamesaidia Mamlaka ya Utalii ya Bamuda kuboresha uwepo wake mtandaoni kwenye huduma ya Ramani za Google na kuendeleza upatikanaji wa biashara za karibu. Pia wamewasaidia watalii kugundua Bamuda mtandaoni wanapopanga (au kutamani!) kusafiri.
Tonga
Waanzilishi wa Grid Pacific, Tania Wolfgramm na Wikuki Kingi, wanarekodi safari yao ya kuweka Tonga kwenye ramani. Ili kukuza utamaduni wa Tonga na visiwa vingine vya pasifiki, walianza mpango mkubwa wa kuweka funguvisiwa lote kwenye ramani na katika Taswira ya Mtaa. Tazama taarifa yao ya kusisimua hapa.