Vyanzo vya picha
Picha za Taswira ya Mtaa hutokana na vyanzo viwili, Google na wachangiaji wetu.
Maudhui Yetu
Maudhui yanayomilikiwa na Google hutaja "Taswira ya Mtaa" au "Ramani za Google." Tunafunika nyuso za watu na nambari za magari katika picha zetu kiotomatiki.
Maudhui kutoka kwa wachangiaji wengine
Maudhui yanayochangishwa na watumiaji huambatana na jina la akaunti unaloweza kubofya au kugusa, na wakati mwingine huwa na picha ya wasifu.
Google inavyokuletea Taswira ya Mtaa
Ili kushiriki picha za Taswira ya Mtaa, timu yetu ya wahandisi hujitahidi sana katika kazi zake. Huu ni muhtasari wa mambo ambayo timu hiyo inafanya ili kukuletea Taswira ya Mtaa.
-
HATUA YA 1
Kukusanya picha
Kwanza tunahitaji kuzunguka na kupiga picha za maeneo ya kuonyesha katika Taswira ya Mtaa. Tunazingatia kwa umakinifu mambo mengi, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa na idadi ya watu katika maeneo mbalimbali, ili kuamua ni lini na wapi tutakapokusanya picha bora iwezekanavyo.
-
HATUA YA 2
Kupanga picha
Ili kulinganisha kila picha na eneo lake la jiografia kwenye ramani, tunatumia kwa pamoja maelezo kutoka kwenye vihisi vilivyo katika magari vinavyopima GPS, kasi na mwelekeo. Hii hutusaidia kuunda upya njia halisi ambayo gari lilipitia na hata kugeuza na kupanga picha upya inavyohitajika.
-
HATUA YA 3
Kugeuza picha ziwe za digrii 360
Ili kuzuia mapengo katika picha za 360, kamera zinazokaribiana hupiga picha zinazoingia katika eneo la picha nyingine kwa kiwango kidogo, kisha "tunaunganisha" picha hizo pamoja kuwa picha moja ya digrii 360. Kisha, tunatumia kanuni maalum za kuchakata picha ili kupunguza "mikunjo" na kuunda mwonekano laini.
-
HATUA YA 4
Kukuonyesha picha sahihi
Kasi ya vile leza tatu za gari zinavyoakisi maeneo hutujulisha umbali wa jengo au kifaa na kutuwezesha kuunda miundo ya 3D. Unaposogea eneo lililo mbali, muundo wa 3D huamua mandhari bora ya kukuonyesha ya eneo hilo.

Tunakokwenda
Tunasafiri katika nchi nyingi kwa magari ya Taswira ya Mtaa ili kukuletea picha zinazoboresha hali yako ya utumiaji na zinazokusaidia ugundue mazingira yako. Angalia orodha ya nchi ambako tutatembelea hivi karibuni.
Kanda | Wilaya | Wakati |
---|---|---|
{[value.region]} | {[value.districts]} | {[value.datestart| date:'MM/yyyy']} - {[value.dateend| date:'MM/yyyy']} |
Kutokana na sababu ambazo hatuwezi kuepuka (hali ya hewa, kufungwa kwa barabara n.k.), inawezekana kuwa magari yetu hayafanyi kazi au huenda tumefanya mabadiliko madogo. Tafadhali kumbuka pia kuwa ikiwa orodha inataja jiji mahususi, huenda tukajumuisha miji na vitongoji ambako tunaweza kufikia kwa gari.
Maeneo ambako tumetembelea
Sehemu za bluu kwenye ramani zinaonyesha mahali huduma ya Taswira za Mtaa inapatikana. Vuta karibu ili upate maelezo zaidi au usome maudhui haya ukitumia programu na tovuti zetu.
Orodha ya magari ya Google ya Taswira ya Mtaa
Pitia orodha ya magari yetu ya Taswira ya Mtaa.
-
Gari la Taswira ya Mtaa
Tumetoka mbali tangu tulipozindua huduma hii mara ya kwanza Marekani mwaka wa 2007; hivi leo tumepanua picha zetu za digrii 360 ili kujumuisha maeneo katika mabara yote saba.
-
Trekker ya Taswira ya Mtaa
Trekker inawezesha Taswira ya Mtaa kujumuisha maeneo zaidi duniani kote - maeneo ambayo hayafikiwi kwa kutumia gari, baiskeli, toroli au gari la theluji. Mkoba huu wa kuvalika mgongoni umefungwa mfumo wa kamera juu, uwezo wake wa kubebeka unatuwezesha kukusanya picha tukipita maeneo madogo au membamba yanayoweza kufikika tu kwa miguu. Shughuli yetu ya kwanza ya ukusanyaji kwa tukitumia teknolojia hii ya kamera ilihusisha mandhari yenye miamba ya mbuga ya Grand Canyon katika Jimbo la Arizona.
-
Toroli ya Taswira ya Mtaa
Wakati kundi la WanaGoogle wanaopenda sanaa walipotaka kupeleka teknolojia ya Taswira ya Mtaa katika majumba ya makumbusho duniani kote, tulihitajika kuunda mfumo ambao ungeweza kutoshea katika milango ya majumba hayo na kuzunguka sanamu kwa urahisi. Katika safari hii ya kwanza ya ndani ya jengo tulifunga vifaa vyote muhimu kwenye fremu ndogo zaidi: mkokoteni wa kusukuma uliofungiwa mfumo wa kamera ulioitwa Toroli. Haujakusanya tu taswira za ndani ya majumba ya makumbusho, bali pia maeneo mengine ya ndani ya majengo kama vile White House na viwanja vya michezo.
-
Gari la Theluji la Taswira ya Mtaa
Sehemu nyingine tuliyodhani ingevutia kupiga picha kwa kutumia kamera za Taswira ya Mtaa ni kwenye miteremko. Baada ya wikendi chache za kutumia magari ya 2X4, utepe wa gundi, na hifadhi zaidi zilizofungwa ndani ya jaketi la kuvaa wakati wa kuteleza kwenye theluji ili kustahimili baridi inayogandisha, timu yetu ilifaulu kufunga vifaa vya Taswira ya Mtaa kwenye gari la theluji. Sasa wanaoteleza kwenye barafu, watelezaji wa bao za theluji na watembeaji kwenye theluji wanaweza kugundua Mlima wa Whistler Blackcomb na mandhari ya theluji ya maeneo yaliyo karibu.
-
Baiskeli ya Magurudumu Matatu ya Taswira ya Mtaa
Kwa miji iliyo na barabara nyembamba ilitubidi tutafute gari thabiti la kushikilia Trekker ya Taswira ya Mtaa. Ili kupitia baadhi ya njia nyembamba, timu yetu iligundua kuwa pikipiki aina ya Selis Robin katika Indonesia zilifanya kazi vyema. Jionee kijigari cha magurudumu mitatu cha Taswira ya Mtaa. Tumeunda nguzo ya ziada inayotumika hasa katika gari hili ili kuimarisha uthabiti wa Trekker ya Taswira ya Mtaa.