Tunasherehekea miaka 15 ya Taswira ya Mtaa
Taswira ya Mtaa ilianzishwa mwaka wa 2007 kutokana na wazo ambalo halikuwa yamkini la kubuni ramani ya digrii 360 ya ulimwengu. Tangu wakati huo, tumepiga zaidi ya picha bilioni 220 na kurekodi zaidi ya maili milioni 10 katika nchi na maeneo 100 kwa jumla.
Katika harakati hizo umegundua anga, bahari na maeneo yanayovutia; na kila mara umepata njia ya kukuelekeza nyumbani.
Gundua maeneo ya kupendeza kwenye Taswira ya Mtaa
-
Tembelea Icefjord nchini Grinlandi
-
Kwea mwamba wa El Capitan katika mbuga ya Yosemite ukiwa na mkwezi mtaalamu
-
Furahia mandhari ya anga ya Paris ukiwa juu ya Mnara wa Eiffel
-
Tazama msikiti mkubwa maarufu wa Sheikh Zayed
-
Tazama kasuku wa kipekee duniani asiyeweza kupaa nchini Nyuzilandi
-
Gundua mahekalu ya zamani ya Machu Picchu
Kuna yapi mapya katika Taswira ya Mtaa?
Zinaonyeshwa sasa: Kumbukumbu za safari
Sasa unaweza kuona jinsi maeneo yamebadilika kadri ambavyo muda umepita kwa kutumia picha za kumbukumbu kwenye Taswira ya Mtaa katika programu ya Ramani za Google.
Pakua programu ya Ramani za Google
Mandhari 15 yanayovutia
Angalia baadhi ya matukio na mandhari yanayovutia zaidi yaliyo kwenye sayari yetu, kama vile Sherehe za Barafu za Mongolia na makazi yanayoelea kwenye Ziwa Titicaca.